DAR ES SALAAM-Timu ya Taifa ya Wanawake U20 (Tanzanite) imeibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Djibouti katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2024 nchini Colombia.
Mtanange huo umepigwa Oktoba 8, 2023 katika Uwanja wa Azam Complex katika Kata ya Chamanzi uliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Jamila Rajab ndiye alitupia mawili nyavuni, Noela Luhala,Winfrida Gerlad na Yasinta Joseph wakamalizia ushindi huo.
Aidha,timu hizo zitarudiana Jumatano hapo hapo Azam Complex Djibouti akiwa mwenyeji na mshindi wa jumla atakutana na Nigeria katika Raundi ya Tatu ya mbio za nchini Colombia 2024.