Trafiki wa Saudia Arabia waanza msako kwa wasiokuwa na bima halali za magari

JEDDAH-Oktoba Mosi, 2023 Idara Kuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Saudia Arabia imeanza kutekeleza mkakati wake wa ufuatiliaji wa moja kwa moja wa ukiukaji wa kutokuwa na bima halali ya magari.

Idara hiyo ya Trafiki ilieleza kuwa, ufuatiliaji huo wa ukiukaji wa sheria na taratibu utatumika moja kwa moja kwa magari yote barabarani na utatumika katika miji na mikoa yote katika Ufalme huo.

Ukiukaji wa gari utafuatiliwa kwa mfumo wa kielektroniki mara moja kila siku 15 katika tukio ambalo gari litaonekana halina bima halali.

Utaratibu wa kuuliza kuhusu uhalali wa bima ya gari unaweza kujulikana kupitia hatua tano kama vile kuingia katika akaunti ya mpokeaji huduma kwenye jukwaa la Absher, kisha kwenda kwa huduma za gari, maswali, na kisha kuchagua uhalali wa bima ya gari.

Hii itafuatiwa na hatua inayojumuisha kujaza sehemu zinazohitajika namba ya kitambulisho na namba ya usajili wa gari, muonekano wa gari, na uhalali wa bima.

Kwa mujibu wa SG ni vyema kutambua kwamba, marekebisho yaliyofanywa katika Sheria ya Trafiki kupitia Amri ya Mfalme hapo awali yalitaja kwamba ukosefu wa bima halali ya gari ni ukiukaji unaohitaji faini ya chini ya Riyal (SR) 100 na kiwango cha juu cha SR150.

Pia, idara hiyo imewatahadharisha na kuwataka madereva wa magari, raia na wageni, kuzingatia kanuni na maelekezo ya trafiki, pamoja na kuhakikisha vyombo vyao vinakuwa na bima halali ili kulinda haki zao pindi ajali zinapotokea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news