ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameanza ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo kuelekea shamrashamra za miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Nane madarakani.
Oktoba 23, 2023 Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amefungua Hospitali ya Kivunge baadae aliweka jiwe la msingi katika ujenzi unaoendelea wa Skuli ya Ghorofa Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais Dkt.Mwinyi amesema, Serikali imekuja na utaratibu mpya wa kushirikisha sekta binafsi katika kutoa huduma kwa hospitali za Serikali ikiwemo maabara, utoaji wa dawa, huduma za Xray na Ultra sound, chakula pamoja na usafi lengo ni kutoa huduma bora za kisasa na za haraka kwa wananchi.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo wakati akifungua rasmi Hospitali ya Wilaya ya Kivunge, Wilaya ya Kaskazini "A" Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amewahakikishia wananchi Serikali itaendelea kujenga skuli za msingi na sekondari za ghorofa kwa pesa ya Serikali, ujenzi wa barabara, miradi ya maji na miradi ya maendeleo yote kwa pesa za Serikali.
Rais Dkt.Mwinyi amesema, wapigaji makelele wachache ni wale wabadhirifu na mafisadi ambao mirija yao imezibwa kwa sasa Serikali malengo yake fedha zinakwenda kwenye miradi ya huduma za kijamii, mishahara ya wafanyakazi wa Serikali, pensheni kwa wastaafu na jamii.