Lengo la mkutano huo ulikuwa ni kutathmini utekelezaji wa Sera ya Fedha na mwenendo na mwelekeo wa uchumi.
Kwa upande wa Zanzibar, ukusanyaji wa mapato ulivuka lengo kwa asilimia 1.7. Matumizi ya Serikali yameendelea kufanyika kulingana na mapato.
Vile vile. Gavana Tutuba amefafanua kuwa. nakisi ya urari wa biashara, huduma na uhamisho mali nje ya nchi imeendelea kuwa kubwa kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa katika Soko la Dunia.
"Hata hivyo nakisi hii ilipungua kufikia dola milioni 3,652.6 kwa mwaka unaoishia Septemba 2023, kutoka dola milioni 4,728.1 kwa mwaka ulioishia Septemba 2022, kutokana na ongezeko la mapato yanayotokana na shughuli za utalii.
"Nakisi hii inatarajiwa kupungua zaidi kutokana na kuendelea kuongezeka kwa mapato yatokanayo na shughuli za utalii, mauzo ya dhahabu na mazao ya biashara nje ya nchi."
Gavana Tutuba amebainisha kuwa, kwa upande wa Zanzibar nakisi ya urari wa biashara,huduma na uhamisho mali nje ya nchi ilifikia dola za Marekani milioni 417.1 ukilinganisha na dola za marekani milioni 344.4, kutokana na ongezeko la gharama za uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi.
Wakati huo huo, MPC imebainisha kuwa, utekelezaji wa sera ya fedha,
pamoja na sera thabiti za kibajeti, na kimfumo, zimesaidia kukabiliana
na shinikizo la mfumuko wa bei, kuchangia ukuaji wa shughuli za kiuchumi
na uhimilivu wa sekta ya fedha nchini licha ya mtikisiko wa kiuchumi
duniani.
Aidha, utekelezaji wa sera ya fedha pia umesaidia
kupunguza shinikizo linalotokana na ongezeko la mahitaji ya fedha za
kigeni nchini.
Kamati pia, ilitathmini mwenendo wa uchumi wa
dunia kwa mwaka 2023 na kubaini kuwa, uchumi wa dunia bado haujaimarika
licha ya ukuaji wa juu ya matarajio uliofikiwa katika kipindi cha nusu
ya kwanza ya mwaka.

Mbali na hayo, kwa kuzingatia mwenendo wa uchumi wa dunia na wa hapa nchini, Kamati ya Sera ya Fedha iliamua kuendelea na utekelezaji wa sera ya fedha inayolenga kupunguza kasi ya ongezeko la ukwasi katika uchumi.
Pia, amebainisha kuwa, Sera ya fedha itaendelea kutekelezwa sambamba na sera za kibajeti na kimuundo ili kufikia malengo ya kiuchumi.
Aidha,amesema utekelezaji wa Sera ya Fedha unalenga kuhakikisha malengo yaliyoainishwa kwenye programu ya Extended Credit Facility (ECF) kwa robo inayoishia Desemba 2023 yanafikiwa.