Wanahabari watakiwa kujikita katika fursa zilizopo Afrika

NA IMMACULATE MAKILIKA
MAELEZO, Misri

WANAHABARI wa Afrika wametakiwa kubadili mitazamo yao kuhusu fursa zilizopo Afrika ikiwa ni pamoja na kulisaidia bara hilo.

Akizungumza na Wanahabari kutoka nchi za Afrika wakati akifungua Mafunzo kuhusu Utangazaji kwa nchi za Afrika (Anglophone Broadcasters) jijini Cairo nchini Misri, Rais wa Baraza Kuu la Usimamizi wa Vyombo vya Habari nchini humo (Supreme Council for Media Regurations), Bw. Salehe El Salhy amesema kuwa, ni wakati sahihi sasa kwa Wanahabari wa Afrika kueleza fursa zilizopo katika bara hilo kwa manufaa ya vijana na Afrika kwa ujumla.

“Wanahabari tuna jukumu la kuisaidia Afrika, vyombo vya habari vinatakiwa kutangaza taswira nzuri ya bara hili pamoja na kueleza fursa zilizopo kwa manufaa ya vijana,"ameeleza Bw. Salehe.

Amefafanua kuwa Bara la Afrika limekuwa na historia ya kutawaliwa miaka ya nyuma na hivyo changamoto kadhaa zimeendelea kuwepo ikiwa ni athari za ukoloni.

Aidha, mafunzo hayo kwa Wanahabari wa Afrika yaliyoanza leo nchini humo yana lengo la kuinganisha Afrika na kutangaza mafanikio ya bara hilo ikiwemo maendeleo na raslimali zalizopo kwa ajili ya watu wa bara hilo.

Mafunzo hayo yameudhuriwa na Wanahabari kutoka nchi nane ambazo ni Tanzania, Namibia, Zambia, Zimbabwe, Liberia, Malawi, Mauritius and Siera Leone.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news