Watoa huduma ngazi ya jamii kutambulika kimuundo

DODOMA-Serikali imepanga kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kuboresha huduma za afya kwa kuweka muundo utakaowatambua wahudumu wa afya ngazi ya jamii.
Hayo yamebainika katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma kilichowahusisha viongozi wa Wizara ya Afya akiwepo Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, Naibu Waziri Dkt. Godwin Mollel, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Grace Magembe, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu pamoja na wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za kimataifa zikiwemo WHO, USAID, UNICEF, AMREF, CDC, PEPFAR na wengineo.

Akiongoza kikao hicho, Waziri Ummy amesema Ssrikali inaendelea kuboresha huduma za afya ngazi ya jamii hivyo wahudumu wamewekewa mkakati wa mafunzo maalum yatkayowasaidia kutoa huduma bora katika jamii inayowazunguka ikiwemo huduma za kinga.

Waziri Ummy amesema, ili kufikia lengo hilo, Serikali haina budi kushirikiana na wadau wa maendeleo ikiwemo taasisi za kimataifa ili ziweze kufadhili mpango huo katika maeneo ambayo wataona yanafaa.

Wahudumu wa afya ngazi ya jamii ni wataalamu wa afya ambao hutoa huduma za msingi kwa jamii yao, kama vile elimu ya afya, kinga ya magonjwa, na matunzo ya kimsingi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news