TANGA-Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Almachius Mchunguzi amesema,kwa sasa jeshi hilo linaendelea kufanya msako kuhusu uingizwaji wa dawa za kulevya na tayari baadhi ya watumiaji wameshatiwa mbaroni.
ACP Mchunguzi amesema,wanaohitajika zaidi ni wale ambao wanauza kwani bila kuwakamata wao biashara hiyo haitakoma. Ameyasema hayo wakati wa matembezi maalumu ya kulinda amani ya jeshi hilo mkoani Tanga.
"Mpango wa kudhibiti dawa za kulevya tunaendelea nao na tayari wapo watu wameshakamatwa, mkoa wetu ni njia ya kupitishia, lakini tunapokamata watumiaji tu haitoshi, inatupasa tupambane na wale wakubwa ambao ni wauzaji ili tuweze kukomesha vitendo hivi.
"Baadhi yao tuna majina yao, sasa niwaambie tu wajisalimishe hata kwa kujitetea, lakini kwa watakaendelea msako wetu utakapompitia kitakachotokea ni maumivu kwake kwa kuwa amekataa kutii sheria bila shuruti,"amesema.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Jeshi la Polisi Tanzania
Kata Dawa za Kulevya
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)