Waziri Dkt.Jafo azindua Mpango wa Utafiti wa Mabadiliko ya Tabianchi

DAR ES SALAAM-Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa rai kwa watafiti kufanya tafiti zitakazosaidia kupata ufumbuzi wa changamoto za kimazingira hususani mabadiliko ya tabianchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa masuala ya utafiti wakati wa hafla ya uzinduzi wa Programu ya Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) leo Oktoba 11, 2023 jijini Dar es Salaam.(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS).

Ametoa rai hiyo wakati akizindua Programu ya Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) leo Oktoba 11, 2023 jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo Tanzania imenufaika na zaidi ya shilingi bilioni 9 zilizotolewa na Serikali ya Norway kupitia Shirika la Maendeleo la NORAD katika makubaliano yaliyosainiwa na Serikali hizo mbili kwa ajili ya kufanya utafiti huo.

Waziri Jafo amesema kuwa uchumi unaweza ukaathirika kutokana na changamoto za kimazingira ambapo jamii hushindwa kufanya shughuli za kujipatia kipato ikiwemo kilimo na ufugaji kutokana na ukame.

Amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo watafiti wanatarajiwa kutoa majawabu kuhusu sekta gani itasaidia katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu na Mkurugenzi Msaidizi katika Kitengo cha Utafiti Elimu ya Juu Bi. Solbjorg Sjoveian wakisaini makubaliano ya ushirikiano katika ufafiti wakati wa hafla ya uzinduzi wa Programu ya Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) leo Oktoba 11, 2023 jijini Dar es Salaam.

“Maeneo haya tuna kazi kubwa ya kujua ni tafiti zipi kwa mfano kama ni kilimo gani kinaweza kufanyika katika maeneo yanayokabiliwa na athari za mabadiliko ya tabianchi, ninyi watafiti mna jukumu kubwa la kutusaidia katika hili,” amesema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) leo Oktoba 11, 2023 jijini Dar es Salaam.

Ameishukuru Serikali ya Norway kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kusema kuwa hayo ni matunda ya diplomasia ya Mwanamazingira namba moja Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Niwapongeze COSTECH na Serikali ya Norway kwa kushirikiana na Tanzania kwa upande wa research (utafiti) kwasababu tuna changamoto kubwa za athari za mabadiliko ya tabianchi na ndio maana tulijiwekea malengo ya kupungunguza emission ifikapo kwa asilimia 30 hadi 35,” amesema.
Wadau wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Programu ya Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ulioongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo leo Oktoba 11, 2023 jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wao Mwenyekiti wa Bodi ya COSTECH Prof. Makenya Maboko pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungua wamesema hatua hiyo imefikiwa kutokana na ushirkiano mzuri baina ya nchi hizo mbili.

Wameshukuru Serikali ya Norway kupitia NORAD na kusema kuwa fedha zilizotolewa zitaleta tija katika hatua ya utafiti Kufanya utafiti.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news