DAR ES SALAAM-Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Prof. Saudin Mwakaje jijini Dar es Salaaam.

Kwa upande wake Prof.Mwakaje amemshukuru RaisDkt. Samia Suluhu Hassan kwa nafasialiyompatia ya kuongoza Baraza hilo kwa nafasi ya Mwenyekiti na kuahidi kusimamia Baraza hilo kutekeleza majukumu yake ipasavyo, kwa kuwasaidia wasanii kunufaika na kazi zao pamoja na kuongeza mapato kwa Serikali.