Waziri Makamba atua India kuelekea ziara ya Rais Dkt.Samia

NEW DELHI-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Dkt.Subrahmanyam Jaishankar ikiwa ni maandalizi ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atakayoifanya nchini humo kuanzia tarehe 8 hadi 11 Oktoba 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Dkt.Subrahmanam Jaishankar ikiwa ni maandalizi ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atakayoifanya nchini humo kuanzia tarehe 8 hadi 11 Oktoba 2023. Mazungumzo yao yalifanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya India jijini New Delhi.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika hivi karibuni jijini New Delhi, viongozi hao pamoja na mambo mengine wamelezea matarajio yao ya kuimarika zaidi kwa ushirikiano kati ya Tanzania na India kupitia ziara hiyo ya kihistoria.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akizunguza na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe.Binaya Srikanta Pradhan jijini New Delhi kabla ya Mhe. Makamba kukutana na Waziri wa mambo ya Nje wa India, Mhe. Dkt. Jaishankar.

Kwa upande wake , Mhe. Makamba amemshukuru mwenyeji wake kwa kumkaribisha nchini humo lakini pia kwa maandalizi mazuri ya ziara ya Mhe. Rais Dkt. Samia nchini humo.

Kadhalika, Mawaziri hao walibadilishana taarifa kuhusu ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili na kukubaliana kuongeza jitihada ili kufikia malengo ya pamoja ya kuinua kuwango cha biashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili na kuhakikisha ushirikiano uliopo unazaa matokeo tarajiwa.
Mhe. Waziri Makamba akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega wakati wa kikao cha kupokea taarifa kuhusu ushirikiano wa Tanzania na India mara baada ya Mhe. Makamba kuwasili nchini India tarehe 6 Oktoba 2023 kwa ajili ya kutathmini na kukamilisha maandalizi ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini humo kuanzia tarehe 8 hadi 11 Oktoba 2023.

Mhe. Rais Dkt. Samia anatarajiwa kuwasili India tarehe 8 Oktoba 2023 kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu.

Wakati wa ziara hiyo kutashuhudiwa ubadilishanaji wa mikataba mbalimbali ya ushirikiano katika sekta za uwekezaji, uchukuzi, afya, maji na nyingine nyingi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. John Kambona (kulia) akiwa na Afisa Mwandamizi wa Idara hiyo Bi. Eliet Magogo na Katibu wa Mhe. Waziri Makamba, Bw. Seif Kamtunda wakati wa kikao cha ujumbe wa Tanzania na Mhe. Waziir Makamba (hayupo pichani) jijini New Delhi kuelekea ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini India tarehe 8 hadi 11 Oktoba 2023.
Mhe. Makamba akizungumza na Mkurugenzi wa masuala ya ushirikiano wa India na Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya India mara baada ya kuwasili nchini humo kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya ziara ya Mhe. Rais Dkt. Samia. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega.
Picha ya pamoja.
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega (kulia) akiwa na Mkrugenzi wa Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga (kushoto) wakati wa kikao na Mhe. Waziri Makamba (hayupo pichani) baada ya kuwasili nchini India. Wengine katika picha ni Mkuu wa utawala Ubalozini, Bw. Deogratius Dotto na Afisa Mwandamizi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Bi. Latifah.

Ziara hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na India hususan kwenye maeneo ya kimkakati na manufaa kwa Tanzania ikiwemo afya, maji, elimu uchumi wa buluu, teknolojia, kilimo, na biashara na uwekezaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news