Acheni undumilakuwili-Padri Masanja

NA ADELADIUS MAKWEGA

“Maana wao unena,lakini hawatendi.” Hayo yalikuwa maneno ya utangulizi ya mahubiri katika Kanisa la Bikira Maria Malkia wa Wamisionari ndani ya misa ya Kwanza ya Jumapili ya Novemba 5, 2023.

“Tunapofakari Injili ya leo , yenyewe inaitupa hadharani shutuma kwa Waadishi an Mafarisayo ambao wameketi katika kiti cha Musa,-wameketi katika nafasi ya kufundisha, nafasi ya kuongoza na nafasi ya kuelekeza, hasa hasa yale yaliyo mafundisho ya Mungu. Licha ya wao kukaa katika nafasi hiyo lakini utendaji wao hauakisi mafundisho hayo, matendo yao hayafanani na yale yanayofundishwa na ndiyo maana Yesu katika injili ya leo Mt 23,1-12 anasema kwa maneno yao muyapokee lakini msiishi kama matendo yao yalivyo.”

Hayo yamesemwa na Padri Samson Masanja , Paroko wa Parokia ya Malya , Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, katika misa ya Jumapili ya Dominika 31 ya Mwaka A wa Liturjia ya Kanisa.

Padri Masanja alihubiri kuwa Kristo ameyasema hayo maana alijua kabisa namna Mafarisayo na Waandishi wanavyoishi . Padri Masanja aliigeuza shilingi ya mahubiri hayo kwa waamini wake na kunadi kuwa,

“Tunaweza kuona kuwa jambo hili ni la Mafarisayo na waandishi tu, Je kwetu jambo hili halituhusu? Jambo hili ni letu pia, sisi mara nyingi tumekuwa wazungumzaji na waelekezaji wazuri lakini tumekuwa hatuyaishi hayo tunayoyasema , hayo tunaelekezwa kuyaishi tunayoyasema na kutokufanya hivyo ni usaliti na ni undumakuwili/undumilakuwili.Tukiishi hivyo hivyo itakuwa kama kama kwa wale Mafarisayo an Waandishi nyakati za Yesu, hapo itakuwa shida maana hata wale wanaotuona watakwazika kwa matendo yetu.”

Mara baada ya kuhitimisha mahubiri hayo ya misa hiyo ya dominika hii, Misa Takatifu iliendelea huku ikiambatana na nia na maombi kadhaa.

“Eee Mungu Baba, mamlaka yanaleta hatari ya kuwaonea wadogo, uwape viongozi wetu moyo wa kutumia mamlaka yako kuwasaidia wanyonge Ee Bwana Twakuomba Utusikie.” Hadi misa hiyo ya domnika inamalizika majira ya saa moja ya asubuhi, hali ya hewa ya Malya na viunga vyake ni ya Jua na Mvua huku mahindi yaliyopandwa mapema yakiwa yamefikia urefu wa zaidi ya sentimeta 30.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news