TANGA-Katibu Mkuu wa Alliance for Democratic Change (ADC) Dira ya Mabadiliko,Doyo Hassan Doyo ametoa wito kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya nchini (NHIF) ili kukidhi mahitaji ya kujihudumia kiafya kwani kufanya hivyo kutasaidia wananchi wengi kupata huduma ya afya kwa urahisi zaidi na kwa ufanisi.
Ametoa wito huo leo jijini Tanga alipokuwa anazungumza na wanahabari katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo.
Doyo ameyasema hayo baada ya kutakiwa kutoa maoni yake juu ya uboreshaji wa huduma za afya hapa nchini.
Aidha,ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa namna inavyoboresha huduma za afya kote nchini, pamoja na hayo Doyo ameiomba serikali kuangalia upya sera yake ya afya ya kuchangia vifaa, huduma tiba kabla ya huduma ili kumsaidia mtanzania kuwahi kupata huduma na baada ya huduma ndugu wa mgonjwa waweze kufanya malipo.
Doyo amesema,kwa kufanya hivyo kutarahisisha matibabu ya wagonjwa na kuwanusuru na mateso ya ugonjwa wakati wakisubiria malipo yafanyike ndipo wapate tiba.