ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, wakati wa kuadhimisha miaka mitatu ya uongozi wake azma yake ya kuifungua Pemba kiuchumi inakwenda vizuri.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo wakati akizindua boti mpya ya Zanzibar 3 ya Kampuni ya Zan Fast Ferries itakayofanya safari zake Pemba hadi Unguja kwa muda wa saa mbili, Tanga na Dar es Salaam.
Mheshimiwa Rais amefanya uzinduzi huo Novemba 1, 2023 katika Bandari ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba
Rais Dk.Mwinyi amesema, alizungumza na wawekezaji mbalimbali kuhusu changamoto ya usafiri Pemba wa anga na bahari hatimaye wawekezaji hao wameitikia wito ikiwemo Kampuni ya Azam Marine, na tayari Zan Fast Ferries wameleta boti mpya ya Zanzibar 3 kwa safari za Pemba. Pia kampuni za Flight link na Assalam Air kuongeza ndege kwa safari za Pemba.