Balozi Naimi Aziz awasilisha Hati za Utambulisho kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNOV na UNODC

VIENNA-Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria na katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Vienna na Mashirika mengineyo ya Kimataifa, Mhe. Naimi Aziz amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Vienna (UNOV) na Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC), Mhe. Ghada Fathi Waly tarehe 24 Novemba 2023.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Balozi Naimi alishukuru UN na UNODC kwa mchango mkubwa wanaofanya katika mapambano dhidi ya uhalifu unaovuka mipaka ikiwemo udhibiti wa biashara ya dawa za kulevya, rushwa, uhalifu wa mtandao, usafirishaji haramu wa watu, silaha, ujambazi pamoja na utakatishaji fedha.

Aidha, wamekubaliana kuendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na UNODC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news