BOOST 'yaiboost' Tume ya Utumishi wa Walimu

DAR ES SALAAM-Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bi. Paulina Mkwama amesema kupitia mradi wa kuboresha elimu ya awali na msingi wameweza kununua kompyuta mpakato 159 kwa gharama ya shilingi milioni 375.

Bi. Mkwama ameyasema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi gari, pikipiki na kompyuta mpakato kwa ajili ya Katibu Wasaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu iliyofanyika leo Novemba 27,2023 kwenye Shule ya Sekondari ya Tambaza mkoani Dar es Salaam.

Amesema,wana mfumo wa kielektroniki wa Tume ya Utumishi wa Walimu ambao usaidia kuhifadhi na kuchatakata taarifa mbalimbali za walimu nchini.
"Ili Makatibu Wasaidizi waweze kuutumia vizuri ni vyema wapatiwe vitendea kazi ambavyo ndio hizi kompyuta mpakato, hivyo kwa sasa tutakua na uhakika wa upatikanaji wa taarifa safi za walimu kutoka kwenye halmashauri zote nchini."

Katika hafla hiyo,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI,Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amekabidhi gari moja aina ya Toyota Coaster, Pikipiki 62 pamoja na kompyuta mpakato 159.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news