DCEA yanasa watuhumiwa wakitengeza biskuti za bangi iliyosindikwa Kawe jijini Dar es Salaam

NA GODFREY NNKO

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imewakamata watu wanaojihusisha na utengenezaji biskuti kwa kuchanganya na skanka (bangi kali iliyosindikwa) maeneo ya Kawe jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo Novemba 8,2023 na Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo, Aretas Lyimo wakati akizungumza na wanahabari katika ofisi ya mamlaka hiyo jijini humo.

"Katika tukio hilo watuhumiwa walikuwa wakiendelea na uzalishaji wa biskuti hizo kwa kutumia mtambo mdogo wa kusaga skanka na vifaa vya kutengenezea biskuti za bangi,"amesema Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo, Aretas Lyimo.

Pia, amesema mamlaka hiyo imebaini maeneo yanayotumika kama masoko ya kuuza skanka hiyo katika ufukwe wa Bahari ya Hindi.

Kamishna Jenerali Lyimo amesema, kupitia operesheni za mamlaka hiyo tayari inashikilia watu 16 huku sita wakiwa wamefikishwa mahakamani na 10 watafikishwa wakati wowote taratibu za kisheria zikikamilika.

Vile vile, mamlaka hiyo kupitia operesheni zilizofanyika kwenye mipaka na fukwe za Bahari ya Hindi imekamata bangi iliyosindikwa kilo 423.54.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news