ZANZIBAR-Imeelezwa kwamba Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi ambayo inatekelezwa kwa pamoja kati ya Serikali na International Fund for Agricultural Development (IFAD) Tanzania Bara na Zanzibar itachangia katika kutekeleza mipango iliyopo ya kitaifa.
Ni kwa kutumia rasilimali zilizopo hususan katika Uchumi wa Buluu ambapo huchangia kwa kiasi kikubwa katika kipato cha wananchi na hatimaye Taifa kunufaika kiuchumi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Dkt. Islam Mchenga akizungumza na Ujumbe wa IFAD uliomtembelea ofisini Kwake Mjini Unguja Zanzibar.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt.Islam Mchenga wakati akizungumza na ujumbe wa IFAD pamoja na Timu ya Uratibu wa Programu ya AFDP Ofisini Kwake Mjini Unguja, Zanzibar.

“Tunaelewa kwa upande wa uvuvi wa bahari kuu, kuna ununuzi wa meli unaoendelea, tukiwa na meli zetu itaongeza tija kubwa kiuchumi na wananchi kuweza kujiajiri,” alieleza.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Dkt. Islam Mchenga akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa shirika la IFAD uliomtembelea Ofisini Kwake Mjini Unguja Zanzibar.
"Tumefanya vizuri katika kilimo cha mwani; ni vizuri tunaweze kuona ni namna gani ya kuweza kubadilishana uzoefu na wenzetu wa Tanzania Bara, ili waweze kunufaika na hizo fursa zilizopo."

Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu Dkt Aboud Suleimani Jumbe akizunguma na Ujumbe wa shirika la IFAD uliomtembelea Ofisini kwake Mjini Unguja Zanzibar.
Ujumbe huo wa (IFAD) umetembelea pia Ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi na utatembelea maeneo mengine yanayotekeleza Programu ya AFDP Zanzibar.