Jamii yaaswa kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara

DAR ES SALAAM-Mkurugenzi Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dkt. John Rwegasha ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kufanya uchunguzi wa afya mara ili kujua changamoto mapema na kuweza kupata matibabu kwa wakati.

Dkt. Rwegasha ameyasema hayo leo wakati akiongea na wanafunzi Wafiziotherapia wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ambapo amesema MNH iko tayari kuwasaidia kwani kundi hilo ni muhimu katika Sekta ya Afya.

“Jumla ya wananchi 150 wameonwa na kufanyiwa uchunguzi wa awali ambapo kuna ambao wamekutwa na changamoto mbalimbali na kupewa rufaa ya kwenda MNH kupitia Idara ya Tiba na Utengamao,"amesema Dkt.Rwegasha.



Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi Wafiziotherapia Tanzania Tawi la MUHAS, Bw. Estom Uvambe, amesema sambamba na hilo pia wamefanya uzinduzi wa chama chao chenye lengo la kuwakutanisha wanafunzi wa kada ya wafiziotherapia nchini.

“Tumeona wagonjwa wenye matatizo mbalimbali wakiwemo wenye shida za misuli, mifupa wagonjwa wa kiharusi, watoto wenye shida za makuzi na wale wote wenye maumivu ya magoti na viungo,"amesema Bw. Estom

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news