DAR ES SALAAM-Chama Cha Mapinduzi kimefanya kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa tarehe 29 Novemba 2023 Jijini Dar Es Salaam chini ya Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilijadili hali ya kisiasa ndani ya Chama na nje ya Chama hapa nchini.
Aidha, kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kimefanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine.
Nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa
Mkoa wa Arusha: Wanachama waliojitokeza 89, Walioteuliwa ni:
–Ndugu Dkt. Daniel Mirisho PALLANGYO
Ndugu Loy Thomas SABAYA
Ndugu Solomon Olesendeka KIVUYO
Ndugu Edna Israel KIVUYO
Mkoa wa Mbeya: Wanachama waliojitokeza 48, Walioteuliwa ni:
–Ndugu Felix Jackson lYANIVA
Ndugu Patrick Adkin MWALUNENGE
Ndugu Fatuma Ismail KASENGA
Mkoa wa Mwanza: Wanachama waliojitokeza 109, Walioteuliwa ni:
–Ndugu Michael Lushinge MASANJA (Smart)
Ndugu Sabana Lushu SALINJA
Ndugu Dkt. Anjelina William SAMIKE
Ndugu Elizabeth Watson NYINGI
Ndugu David Mayala MULONGO
Nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya
Wilaya ya Mpanda: Wanachama waliojitokeza 36, Walioteuliwa ni:
–Ndugu Hamis Chande SOUD
Ndugu Joseph Aniseth LWAMBA
Ndugu Josephina Yusuph BARAGA
Ndugu Emmanueli David MANAMBA
Wilaya ya Kusini Unguja: Wanachama waliojitokeza 15, Walioteuliwa ni: –
Ndugu Maryam Suleiman HAJI
Ndugu Ali Timamu HAJI
Ndugu Mohammed Haji HASSAN
Kuhusu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameijulisha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kupokea barua ya kujiuzulu kwake, na ameridhia ombi hilo.
Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kimepongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025.