ROME-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa tarehe 14 Oktoba, 2023 aliwasili jijini Rome, Italia ambapo alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani lililofanyika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) kuanzia Oktoba 16, 2023 hadi Oktoba 20, 2023.
Mkutano huo wa wakuu wa nchi na Serikali uliambatana na maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani pamoja na maadhimisho ya miaka 78 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO)
Jukwaa hilo liliwakutanisha wadau wa kilimo wakiwemo vijana, wakulima, wazalishaji wadogo, watunga sera, wawekezaji katika kilimo na wanasayansi duniani, wote wakiwa na lengo la kuhakikisha kunakuwa na uhakika wa chakula ili kufikia mustakabali bora wa chakula kwa wote na bila kumwacha mtu yoyote nyuma.
Pia, jukwaa hilo liliweka msisitizo kwa nchi husika katika kuchukua hatua za ndani ambazo zinajikita kwenye uvumbuzi, ushirikiano, sayansi, ushirikishwaji wa vijana, wazawa, wanawake na watu walio katika mazingira magumu.