ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali imedhamiria kuleta mapinduzi makubwa katika utoaji wa huduma za afya kwa kufanikisha sekta binafsi kuendesha hospitali za Serikali ikiwemo miundombinu ya kisasa, vifaa tiba, vitendea kazi, upatikanaji wa dawa, mifumo ya kisasa ya tehama pamoja na ongezeko la fedha katika sekta hiyo.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Novemba 1, 2023 wakati akifungua Hospitali ya Wilaya Vitongoji Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Aidha, Rais Dk.Mwinyi amewatoa wasiwasi wafanyakazi wa sekta ya afya kuwa hakuna atakayepoteza kazi kwa sababu sekta binafsi kuingia kuendesha hospitali za Serikali bali watapatiwa ujuzi pia kupitia vifaa vya kisasa ikiwemo mafunzo ya maabara,ICU na huduma mbalimbali za sekta hiyo.
Vilevile Rais, Dkt.Mwinyi ameendelea kusisitiza huduma za afya Zanzibar zitaendelea kutolewa bure kwa wananchi wote.