Mama Mariam Mwinyi aieleza Jumuiya ya Madola namna Serikali ilivyopiga hatua

LONDON-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mhe.Mama Mariam Mwinyi amesema Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi imeonesha juhudi kubwa.
Ni katika kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kuanzishwa kwa Mahakama Maalumu za kushughulikia mashauri ya udhalilishaji wa kijinsia, kuondoshwa dhamana kwa watuhumiwa wa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia na kuharakisha muda wa kusikiliza kesi za udhalilishaji na hukumu.

Mama Mariam Mwinyi amesema hayo akiwasilisha mchango wake katika mkutano wa Viongozi Wanawake ulioandaliwa na Jumuiya ya Madola ukumbi wa Marlborough House, London Uingereza tarehe 15 Novemba 2023.

Aidha, Mama Mariam Mwinyi ameeleza malengo na uzoefu wa Taasisi ya ZMBF katika kuchangia juhudi za Serikali kuinua ustawi wa maisha kwa Wanawake, Vijana na Watoto ikiwemo uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi hususani wakulima wa Mwani, kuimarisha afya ya Mama na mtoto, kuanzisha programu ya kusaidia upatikanaji wa taulo za kike.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news