NA DIRAMAKINI
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Mheshimiwa Dkt.Ritta Kabati amewashauri wananchi, pale wanapofanya uamuzi wa kuwachangua viongozi kwa ajili ya kuwawakilisha katika ngazi mbalimbali za maamuzi wachague watu wenye hofu ya Mungu.
"Nitumieni, nitatumika nina Yesu sasa hivi nimeshachagua fungu la kusoma Biblia ni heri kujipendekeza kwa Yesu, kujipendekeza kwa Yesu kuna faida,"amefafanua Dkt.Kabati.
Dkt.Mjuni
Kwa upande wake,Mtumishi wa Mungu wa Huduma ya Yerusalemu Pomerini Ministry iliyopo Kilolo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa, Nabii Dkt.Mjuni Kisha amempongeza Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Dkt.Ritta Kabati kwa kutambua kuwa, bila Mungu hakuna jambo lolote linalowezekana.
Dkt.Mjuni ametoa pongezi hizo wakati wa hitimisho la mkutano huo huku akimshukuru kwa kuwa mstari wa mbele katika kugusa wenye mahitaji mbalimbali na kuunga mkono neno la Mungu liweze kusonga mbele.

Ushauri huo aliutoa wakati akihitimisha mkutano wa injili ulioandaliwa na Mtumishi wa Mungu wa Huduma ya Yerusalemu Pomerini Ministry iliyopo Kilolo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa, Nabii Dkt.Mjuni Kisha.
Kupitia mkutano huo ambao ulifanyika kati ya Novemba 17 hadi 19, 2023 katika Kijiji cha Ng'uruhe Pomeni Kilolo, Dkt.Kabati ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema,viongozi wenye hofu ya Mungu wana mchango mkubwa katika kuyapatia ufumbuzi wa haraka mahitaji ya wananchi.
"Nina imani siku nyingine nitakuja kiserikali, kwa sababu mimi ni Mbunge wa Mkoa mzima. Na mimi siyo kwamba ni Mbunge labda wa miaka mitatu, sijui Mbunge wa lini, hiki ni kipindi cha tatu, nina ubunge sasa miaka 15 kuwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa mzima.
"Kuna vitu ambavyo nimevifanya ambavyo niliona Mungu amenielekeza nivifanye kwa hiyo ninapokuja hapa kwenu leo hii, kitu kingine ambacho nimekichagua ni kwamba ukimtumikia Mungu siku zote Mungu hatakuacha kwa sababu mimi ni mzee wa kanisa, mimi ninaimba kwaya, nikiwa Dodoma ninaimba, nikiwa Iringa ninaimba, nikiwa Dar es Salaam ninaimba kwaya.
"Kitu ambacho nimejifunza ukimtumikia Mungu hatokuacha na siku zote jitahidini tunapochangua viongozi, chagueni viongozi wenye hofu ya Mungu, sisi viongozi tusiwe viongozi wa kuwaumiza watu.
"Tuwe ni viongozi wa kubariki watu, kwa sababu tunapokuwa tumepata vyeo tunakuwa tumepata fimbo ya kuwapigia wanyonge.
"Kitu ambacho hata Mungu hataki, kwa hiyo siku zote, tunaelekea kwenye uchaguzi sasa wa Serikali za Mitaa, sisi watumishi wa Mungu tupige magoti, Mungu atuchagulie viongozi watakaoongoza nchi hii, viongozi watakaoongoza kata hii.
"Viongozi watakaoongoza kwenye matawi yetu, kuwa ni viongozi wenye hofu ya Mungu ili watende haki kwa wanaowaongoza ndiyo tutakwenda, lakini tukichagua viongozi kwa ajili ya fedha tutaumia wenyewe, tutakula mara moja tu, lakini tutateseka miaka mitano yote.
"Leo hii ninakuja kwenye mkutano wa injili ninamshukuru sana sana Dkt.Mjuni ambaye amesema nije hapa kwenu, ningetamani niongee sana, ningetamani niongee mambo mengi sana, lakini ninajua muda siyo rafiki,lakini ninajua mimi hapa ni kwetu.
"Siku yoyote nitumeni, nimekuwa nikifanya kazi kwenye mkoa mzima wa Iringa nimeshangaa ninaitwa huko Isimani, ninaitwa sijui Mufindi ninaitwa sijui wapi, lakini ninashangaa watu wa nyumbani hawajanitumia sana, nikasema acha nijiseme mwenyewe.

Tags
Acha Injili Iende Mbele
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Habari
Iringa Region
Ritta Kabati