PWANI-Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah amefanya mazungumzo na Uongozi wa Kiwanda cha Marumaru cha Keda na kutembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho kilichopo Chalinze mkoani Pwani.
Katika mazungumzo hayo,Mkurugenzi Mkuu aliuambia Uongozi wa kiwanda hicho kuwa NHC inatembelea viwanda mbalimbali kuona uwezo, gharama na muda utakaotumika kuzalisha vifaa vya ujenzi vitakavyosaidia NHC kujenga nyumba za gharama nafuu kwa Watanzania.


Ziara hii ni muendelezo wa ziara mbalimbali zinazofanywa na NHC katika viwanda vya kutengeneza vifaa vya ujenzi.