Msitupangie, tunasonga mbele-Netanyahu

TEL AVIV-Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amefutilia mbali usitishaji vita kwa muda huko Ukanda wa Gaza hadi Hamas iwaachilie mateka wake zaidi ya 240.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu (kulia) akiwa na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Antony Blinken. (Picha na @SecBlinken).

Uamuzi huo unarudisha nyuma shinikizo la Marekani la kusitishwa kwa uvunjivu wa haki za kibinadamu ikiwemo kulinda raia na kuruhusu msaada katika eneo hilo lililozingirwa.

Hayo yalijiri ikiwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken aliwasili Israel siku ya Ijumaa ili kutoa wito wa hatua za kuwalinda raia na kuruhusu misaada zaidi kuingia Gaza, huku wanajeshi wa Israel wakiuzingira mji mkuu wa eneo hilo baada ya siku kadhaa za kuzidisha operesheni za ardhini.

Netanyahu amemwambia Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Antony Blinken kuwa Israel haina nia ya kukubali usitishwaji wa mapigano ingwa Marekani inataka vita visitishwe ili misaada ifike Gaza.

Akizungumza baada ya kukutana na Blinken, Netanyahu amesema aliweka wazi kuwa wataendelea kusonga mbele kwa nguvu zote.

Pia, Waziri Mkuu huyo amesema,wanakataa usitishwaji wowote wa mapigano ambao hautajumuisha kuachiwa kwa mateka wao.

Maafisa wa Israel wanakadiria kuwa karibu watu 249 walitekwa katika mashambulizi ya Oktoba 7, mwaka huu na wanashikiliwa mateka Gaza.

Umoja wa Mataifa unazingatia usitishwaji wa mapigano kwa ajili ya kupelekwa misaada kuwa ni mpango wa muda mfupi unaofikiwa na pande zote ili misaada ifikishwe katika eneo maalum kwa muda maalum.

Aidha,kusitishwa mapigano, kwa upande mwingine, ni mpango wa muda mrefu na hasa huwa sehemu ya mchakato wa kisiasa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken alikutana na Rais wa Israel, Isaac Herzog jijini Tel Aviv, akisisitiza kuwa ,Israel ina haki ya kujilinda, wakati akizungumzia haja ya kuongeza kwa kiasi kikubwa na haraka msaada endelevu katika Ukanda wa Gaza.

Blinken vilevile alisisitiza kuhusu ulinzi wa raia wa Gaza ambao wamenaswa katika makabiliano hayo yaliyochochewa na Hamas, akisisitiza kuwa kila kitu kifanywe kuwalinda na kupeleka msaada kwa wale wanaouhitaji kwa dharura na ambao kwa njia yoyote ile hawahusiki na matukio ya Oktoba 7, mwaka huu.

Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu hotuba ya kiongozi mkuu wa Hezbollah Sayyed Hassan Nasrallah, Blinken alisisitiza kuwa Marekani imedhamiria kuhakikisha kuwa hakuna upande wa pili na wa tatu katika mzozo huo.

Waziri huyo alisema Marekani iko katika hali ya tahadhari kubwa katika upande wa Kaskazini, kujibu tukio lolote linaloweza kutokekea kwa sasa na katika siku zijazo kuhusiana na Lebanon, Hezbollah au Iran.

Sayyed alionya kuwa, vita kati ya Israel na Hamas vinaweza kugeuka kuwa mzozo wa kikanda kama mashambulizi yataendelea Gaza. (Agencies)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news