Mtume Dkt.Peter Nyaga kugawa misaada, mitaji kwa watu 1,000 Kanisa la RGC Miracle Centre Tabata

DAR ES SALAAM- Zaidi ya watu 1000 wenye mahitaji maalumu kutoka ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam wanatarajiwa kupatiwa misaada, mitaji na huduma nyingine Desemba 3, 2023.

Hayo yamesemwa leo na Balozi wa Amani Duniani ambaye pia ni Mtume na Nabii Dkt.Peter Njue Nyaga wa Urejesho TV Africa na Kanisa la RGC Miracle Centre lililopo Tabata Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Mtume na Nabii Dkt.Peter Nyaga amekuwa akitoa misaada kwa maelfu ya wajane, walemavu, vikongwe, yatima na watu wasiojiweza katika kipindi cha miaka 17.
















"Na Desemba 2, 2023 nitagawa misaada kwa watu 1,000. Wengine watapewa vyakula, wengine watapewa mitaji ya biashara na vitu mbalimbali, tukio hili la kihistoria litafanyika ndani ya Kanisa la RGC Miracle Centre Tabata Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

"Wakazi wote wa Dar es Salaam, msipange kukosa na itakuwa ni siku tatu tarehe 1 itakuwa ni siku ya kongamano, tarehe 2 itakuwa ni siku ya kongamano na tarehe 3 ni sherehe kubwa ambapo chakula cha mchana, vinywaji vitatolewa bure.

"Na wajane, viwete, yaani watu wenye ulemavu wakiwemo Albino, na watu wasiojiweza zaidi ya 1000 watapewa misaada.

"Kama unahitaji kusapoti huduma hii ili tuweze kuwapatia wahitaji wengi zaidi mahitai siku hiyo unaweza kutuma sapoti yako ya sadaka kupitia Tigo Pesa namba 0716 147361 nami Mtume Dkt.Petr Nyaga nitapokea na kukuombea,"amesema Nabii na Mtume Dkt.Nyaga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news