DAR ES SALAAM-Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wamefanikiwa kutoa kipande cha plastiki kwenye pafu la kushoto la mtoto mwenye umri wa miaka 11, kupitia kifaa maalumu kinachoitwa Flexible Bronchoscopy.

Akizungumza kwa niaba ya timu ya watalaam Daktari Bingwa wa Mapafu, Dkt. Mwanaada Kilima amesema kuwa mtoto huyo alikuja na dalili za kikohozi cha muda mrefu na siku zote amekuwa akiambiwa ana homa ya mapafu mpaka alipokuja Muhimbili na kupatiwa matibabu sasa kikohozi kimeacha na hali yake inaendelea vizuri na tunatarajia kumruhusu ili aende nyumbani kuendelea na maisha.
