NAIBU WAZIRI BYABATO AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA KOREA

ARUSHA-Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato, amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea, Bi. Oh Youngju, pembeni mwa Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha.
Katika mazungumzo yao viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea kwa manufaa ya pande zote mbili.

Akizungumza katika mkutano huo Naibu Waziri Mhe. Byabato alimuelezea Bi. Youngju kuridhishwa kwa Tanzania juu ya ushirikiano na uhusiano uliopo kati yake na Jamhuri ya Korea na kuahidi kuendelea kushirikiana na nchi hiyo kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.
Naye Bi. Youngju alimuelezea Naibu Waziri Byabato juu ya mpango wa Jamhuri ya Korea wa kuandaa Mkutanoo kati ya Nchi yake na Viongozi wa Bara la Afrika uliopangwa kufanyika mapema mwezi Juni 2024 na kwamba anaialika rasmi Tanzania ishiriki katika mkutano huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news