NEC yamteua Aziza Sleyum Ally kuwa Mbunge wa Viti Maalum

DAR ES SALAAM-Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) imemteua Aziza Sleyum Ally kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 3, 2023 na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima.

"Katika kikao chake leo tarehe 3 Novemba, 2023. Tume ya Taia ya Uchaguzi kwa kuzingatia matakwa ya Ibara ya 78 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977,

"ikisomwa pamoja na kifungu cha 86A (6) na (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 imemteua ndugu Aziza Sleyum Ally kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)."

Kwa mujibu wa NEC, uteuzi huo umefanyika baada ya tume hiyo kupokea barua yenye Kumb. Na CFA. 137/400/02A/22 ya tarehe 19 Agosti, 2023 kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoandikwa kwa mujibu wa kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Barua hiyo ilikuwa ikiitaarifu tume kuhusu uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufuatia kujiuzulu aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Bahati Keneth Ndingo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news