Prof.Muhongo aimegea Serikali mbinu kupunguza umaskini

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo ameishauri Serikali kuwa mipango ya maendeleo inapaswa kuwa na shabaha ya kupunguza umaskini kwa kiasi kikubwa pamoja na kushughulikia mahitaji muhimu ya kila siku ya Watanzania ikiwemo chakula, maji umeme na matibabu.

Prof. Muhongo ameyasema hayo Novemba 9, 2023 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mapendekezo ya Mpango wa Taifa kwa mwaka wa Fedha wa 2024/2025 ambapo pia amesema kuwa, uchumi wa nchi unapaswa ukue kwa kasi ya asilimia 8-10 ili kupunguza umaskini kwa kasi kubwa.

"Mipango na bajeti zake vishughulikie mahitaji muhimu ya kila siku ya Watanzania kama chakula, maji, umeme na matibabu. Vipimo vya upatikaji wa huduma muhimu kwa vile maji na umeme, viweke maanani matumizi halisi ya mtu mmoja mmoja kwa mwaka,

"Uchumi wetu kwa muda mrefu umekua kati ya asilimia tano na imedhihirika ukuaji huo wa uchumi ambao tumekuwa nao kwa miaka kati ya 20, 30 haujaweza kuondoa kwa kiasi kikubwa umaskini nchini mwetu.

"Kwa hiyo mipango yetu lazima ijielekeze kwenye uchumi unaokua zaidi ya asilimia Sita na duniani kote wamepiga hesabu uchumi huo lazima ukue Kati ya asilimia 8 mpaka asilimia 10."

"Ikifika mwishoni mwa mwaka huu GDP per Capital yetu itakuwa dola 1,113, bado tuko mbali sana kwenye malengo ya dola 3,000.

"Na mpango wetu lazima ujielekeze kwenye kufuta umaskini. Mipango lazima ifute umaskini kwa Hali ya Sasa nchini mwetu takwimu zinaonesha asilimia 18.7 ya watanzania hawa wako below food poverty line yaani matatizo ya chakula,"

"Na kwa matumizi ya kawaida ukichukua kwenye hiyo ngazi ni asilimia 35.7, na ukichukua umaskini wote Sasa na nchi nzima unakuta asilimia 13 Mjini watu sio maskini, asilimia 87 Vijijini ni maskini sana.

"Mapendekezo yangu uchumi wetu ukue Kati ya asilimia 8 hadi 10 na maeneo ya kukuza huo uchumi la kwanza, tuwekeze kwenye uchumi wa gesi asilia Helium, Carbon dioxide na gesi nyingine.

"Miradi yetu ingeeleza sana kwa haraka kutokana na uchumi wa gesi kwenye madini tukiachilia dhahabu, kuna madini ambayo yana thamani sana humo duniani. Pia kwenye Kilimo, Uvuvi, ufugaji na Utalii hivi ni vyanzo vya kipaumbele vya mapato.

"Haya yote kusudi yaweze kufanikiwa lazima tuwe na elimu bora kwa njia zote tumetengeneza sera ambayo itaanza 2027. Lakini nina wasiwasi kwa Halmashauri zetu na mabaraza ya madiwani yanaweza kusimamia utekelezaji wa hiyo sera.

"Elimu bora maana yake tupate Walimu na wakufunzi walio bora, lazima tupate vifaa Bora vya kufundishia na kujifunzia kama maabara, mipango yetu lazima iangalie nchi ambazo zimefanikiwa duniani. Ningechukia duniani South Korea, Finland na Uingereza ambao tumerithi mtindo wao wa elimu.

"Kwa Afrika hapa kwa elimu bora hatujawa hata kwenye tano au nane bora ya kwanza ni South Africa, ya pili ni Kenya na ya tatu ni Botswana. Hebu tujifikirie kwa nini wamasemekana kuwa na elimu bora. Cha pili kwenye mipango yetu ni mambo ya utafiti na ubunifu.

"Hakuna taifa lolote duniani ambalo linasema lina mipango mizuri ya maendeleo bila kuwekeza kwenye research development na innovation na mpango yetu lazima ioneshe maeneo ya kipaumbele,"

"Ningechukua upande wa kilimo, seeds science and technology spaces Science na Nuclear Science na life science kwenye mambo ya matibabu. Mipango yetu lazima ituoneshe hayo pia ioneshe tuna Watafiti wangapi.

"Kwenye bajeti ya utafiti mipango yetu iongee inasemekana kwamba mwaka jana Tanzania tumetumia Dola Mil. 870 lakini majirani zetu Kenya wametumia dola Bilioni 2, na duniani utafiti umetimia zaidi ya trilioni 2.5, kwa hiyo unaona mipango yetu haijaweka mkazo kwenye utafiti,"

"Lazima twende kwenye vitu ambavyo Watanzania wanavitumia kila siku na hapa nachukua vitu vinne tu yaani Chakula, maji, umeme na matibabu. Mipango yetu lazima ishughulikie haya lazima tujue miaka 10 au 20 ijayo tunahi taji Chakula kiasi gani,"

"Kusema kwamba mfano maji Kijiji fulani au Wilaya fulani imefikia asilimia fulani hiyo ni fursa, sio kipimo kizuri kipimo kizuri ni kwamba mtu ametumia maji kiasi gani kwa mwaka hicho ndicho kipimo kizuri na Cha kitaaluma. Yani eneo ambalo mwananchi mmoja mmoja kwa mwaka hatumii zaidi ya lita Mil. moja (1) duniani huko inasemekana Kuna matatizo hapo. ripoti za kusema maji ni asilimia 70 haitoshi,"

"Mingine ni umeme, na hayo yote yako kwenye docoment za UN sustainable development goals yako Africa Union... umeme kwenye umeme nako kuna tatizo hilo hilo. Mtu anasema umeme matumizi sehemu fulani umefika kwa asilimia fulani lakini sio kweli mfano ukisema Musoma Vijijini Kijiji changu kimoja asilimia 75 wanapata umeme hiyo ni fursa umeme umekaribia lakini kipimo kizuri ni umeme kiasi gani mtu anatumia kwa mwaka.

...unakuta unachukua majirani zetu Kenya umeme wanaotumia kwa mwaka unit ni units 180 GDP yao per Capital ya Kenya ni zaidi ya dola 2000.

"Inakuja Tanzania, umeme tunaotumia zile unit ni 99. 6 GDP yetu ni karibu dolla 1,100, kwa hiyo Mimi mapendekezo yangu ni kwamba tuwe na mipango ambayo tukiwekeza kwenye Kilimo, Uvuvi na ufugaji tutapata mara moja lakini tuwe na mipango ya kuwekeza kwenye mabarabara na reli ambapo mapato yake yanaweza kupatikana baada ya muda mrefu."amesema Prof. Muhongo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news