PSSSF Kigoma yapigwa marufuku undelezaji ujenzi Eneo la Ukanda wa Kijani

KIGOMA-Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amepiga marufuku Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuacha mara moja uendelezaji wa jengo lao katika Manispaa ya Kigoma kutokana na mfuko huo kupewa eneo lililohifadhiwa kwa ajili Ukanda wa Kijani.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maeneleo ya Makazi Jerry Silaa akipitia nyaraka mbalimbali wakati wakushughulikia mgogoro wa Ardhi jana katika Manispaa ya Kigoma.

Waziri Silaa amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kusimamisha maendeleo yoyote ya ujenzi katika eneo hilo ikiwemo Ofisi ya Mtendaji Kata pamoja na kuondelewa kwa shughuli nyingine za kijamii na wafanyabiashara ndogondogo.

Waziri Silaa amesema hayo wakati akihitimisha ziara yake siku mbili mkoani Kigoma na kuwataka watendaji wote wa sekta ya ardhi mkoani humo kuzingatia matakwa ya sheria za ardhi ili kila mtu apewe haki yake wakati wa kufuata taratibu za kumiliki ardhi.

Waziri Silaa alisisitiza kuwa, suala PSSSF halihitaji hata yeye kurudi ofisini bali hataki kabisa na hivyo kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma kutoa taarifa kwa viongozi wa mfuko huo ili kutafuta eneo lingine hata kama linahitaji kutolewa fidia akiongeza kuwa shirika hilo ni kubwa.

Agizo la Waziri Silaa pia likawaangazia pia watu wa Takwimu ambao pia wametwaa eneo bila kuwa na hati milki ya eneo husika na kuagiza waandikiwe barua ili viongozi wao wajue kuwa walinunua eneo bila kuwa na hati.

Baadhi ya wananchi wakishuhudia Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa alipofika uwandani kusikiliza utatuzi wa mgogoro wa kiwanja.

"Kama mmegawa eneo lililoifadhiwa kwa namna yoyote mkagawa ofisi ya kata, hiyo ofisi ya kata itavunjwa halafu mtamweleza Waziri wa TAMISEMI kwa nini? Fedha zake zimetumika kujenga katika eneo ambalo sio sahihi kwa matumizi yale ndio maana nakataa mabadiliko ya matumizi ya viwanja,"aliongeza Waziri Silaa.

Waziri Silaa aliongeza kuwa, kama wataalamu wa ardhi wanataka kubadilisha matumizi ya ardhi katika eneo fulani ni vyema wakishirikisha wananchi ili makubaliano yafanyike kwa pamoja ili kila mtu aelewe kusudio hilo kwani wananchi hao pia wana haki ya kupendekeza matumizi wayatakayo.

Waziri Silaa amehitimisha ziara yake mkoani Kigoma na anaendelea na ziara nyingine kama hiyo mkoani Katavi ambapo ataendelea kujionea shughuli mbalimbali mkoani humo ikiwemo utoaji hati kwa wananchi waliokamilisha taratibu za utwaaji ardhi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news