ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi wawili.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said ambapo uteuzi huo umeanza Novemba 20,2023.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Safia Ali Rijaal kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni (BASSFU). Ndugu Safia ni mstaafu wa utumishi wa umma,
Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Profesa Issa Haji Ziddy kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar. Profesa Issa ni mstaafu wa utumishi wa umma.