Rais Dkt.Mwinyi atimiza ahadi zake kwa wajasiriamali

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2020 alikutana na wajasiriamali waliomweleza changamoto kuu nne zinazokwamisha biashara zao.

Miongoni mwa changamoto hizo ni hitaji la mazingira mazuri ya kufanya biashara, ukosefu wa mitaji, ukosefu wa mafunzo pamoja na utaratibu wa kodi katika biashara zao.
Dkt.Mwinyi amesema, kufungua vituo vya wajasiriamali nchini vilivyojengwa na Serikali ni kutimiza yale yaliyoahidiwa kwa kutengeneza mazingira mazuri ya wajasiriamali kufanya biashara zao, kutolewa mikopo kupitia Serikali na benki ya CRDB na kuweka viwango vidogo vya kodi katika vituo hivyo vya wajasiriamali.

Pia amezitaka taasisi za benki na nyinginezo kuendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali nchini. Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Novemba 1,katika hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Wajasiriamali Michakaini Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ametoa ofa ya kutolipa kodi kwa miezi mitatu bure kwa wajasiriamali wa kituo hicho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news