ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj DkT.Hussein Ali Mwinyi amesema amani ndiyo nguzo kuu ya mambo mengine yote bila amani huwezi kuzungumza maendeleo.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Novemba 3, 2023 baada ya kujumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya sala ya Ijumaa Masjid Noor Kombeni, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Vilevile Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa, ni wajibu kuilinda na kuitunza amani ya nchi kwa kila mwananchi na si jukumu la Serikali peke yake kwa kuanzia ngazi ya jamii, pamoja na familia kupitia malezi .