ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar aliowateua hivi karibuni.
Katika hafla hiyo, majaji hao ni Mhe.Khadija Shamte Mzee, Mhe.Salum Hassan Bakari, Mhe.Haji Suleiman Khamis.
Hafla hiyo ilifanyika Ikulu Zanzibar tarehe 16 Novemba 2023.Viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini na Vyombo vya ulinzi na usalama walihudhuria hafla hiyo.