ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewataka watendaji mbalimbali wa sekta ya afya kuhakikisha wanasimamia zoezi la kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo Novemba 2, 2023 alipofungua hospitali ya Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Pia wafanyakazi wa sekta hiyo wajifunze mbinu mpya na ujuzi utakaotolewa na sekta binafsi ambao ni waendeshaji wa hospitali za Serikali pamoja na kambi za madaktari bingwa zitakazokuwa zinafanyika katika kujenga uwezo zaidi.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema kuhusu maslahi ya wafanyakazi wa sekta hiyo litazingatiwa ikiwemo mishahara, posho mbalimbali, kupandishwa madaraja, mafunzo ya nje ya nchi na ndani katika kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wananchi.