DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Mohamed Malick Salum kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).
Bw. Salum anachukua nafasi ya Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 14, 2023 na Zuhura Yunus ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 14, 2023 na Zuhura Yunus ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.