NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Philipo Gekul.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 25, 2023 na Zuhura Yunus ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Utenguzi huo unakuja ikiwa ni miezi kadhaa imepita baada ya Mheshimiwa Rais Dkt.Samia tarehe 26 Februari, 2023 kumhamisha Mheshimiwa Pauline Philipo Gekul kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.