REA yaanza utekelezaji maagizo ya Naibu Waziri Mkuu

NA VERONICA SIMBA
REA

WAKALA wa Nishaji Vijijini (REA) umeanza utekelezaji wa maagizo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa kuwafikishia huduma ya umeme wakazi wa Madimba na Msimbati kwa kufanya tathmini katika maeneo hayo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu (wa pili-kushoto), akijadiliana jambo na Diwani wa Kata ya Msimbati Rashid Linkoni (wa pili - kulia) na Viongozi wengine kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Mwenyekiti na Ujumbe wake walifika eneo hilo Novemba 16, 2023 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa maagizo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko ya kufikisha umeme Msimbati na Madimba.

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Balozi Meja Jenerali Mstaafu,Jacob Kingu alifanya ziara ya kufanya tathimini katika kata za Madimba na Msimbati ili kuona hali halisi kabla ya kuanza utekelezaji.

Naibu Waziri Mkuu, Dkt Doto Biteko, akiwa katika ziara ya kazi mkoani Mtwara hivi karibuni aliitaka REA kuangalia ni namna gani inawezakuwaunganishia umeme wananchi wa maeneo hayo na kujenga miundombinu ili waweze kunufaika na nishati ya gesi asilia inayozalishwa katika eneo hilo.

Akizungumza kwa nyakati tofauti na Madiwani wa Kata za Msimbati na Madimba, Balozi Meja Jenerali Kingu amesema REA itahakikisha maelekezo hayo yanatekelezwa ambapo Novemba 18, 2023 watakutana na mkandarasi kwa ajili ya kujadili ujenzi wa miundombinu ya umeme katika kata hizo.

“Tutahakikisha utekelezaji wa haraka unafanyika na wataalamu wanapitaili kuona hali halisi na uhitaji katika maeneo husika.”

Aliwataka wananchi wa maeneo hayo kuwapatia ushirikiano wataalamu wa REA na mkandarasi ili kuharakisha uratibu wa kazi hiyo.

Ujumbe wa viongozi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakijadiliana jambo na Diwani wa Kata ya Msimbati Rashid Linkoni (wa pili - kulia), wakati viongozi hao walipotembelea eneo hilo Novemba 16, 2023 kwa ajili ya utekelezaji wa maagizo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko ya kupeleka umeme Msimbati na Madimba.

Aidha, alisema Bodi na Menejimenti ya REA watafuatilia kwa karibu utekelezaji wa agizo la Naibu Waziri Mkuu la kuyafikishia maeneo hayo umeme.

Alitaka taarifa zitolewe haraka endapo kutakuwa na changamoto katika utekelezaji wa mradi huo ili zipatiwe ufumbuzi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Nishati Vijijini, Mhandisi Jones Olotu aliwahakikishia Maafisa Watendaji wa Kata hizo mbili kuwa wiki ijayo wakandarasi watafika kukutana nao kwa ajili ya kuoneshwa maeneo na vijiji vinavyotakiwa kufikishiwa umeme.

Alitaka taarifa zitolewe haraka endapo kutakuwa na changamoto katika utekelezaji wa mradi huo ili zipatiwe ufumbuzi.

Diwani wa Kata ya Msimbati, Rashid Linkoni aliishukuru serikali kwa uamuzi wake wa kuhakikisha wanapata umeme na kunufaika na rasilimali ya gesi asilia inayopatikana eneo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news