Saudi Arabia yalaani vikali mauaji huko Jabalia Gaza

GENEVA-Serikali ya Ufalme wa Saudi Arabia imelaani vikali mashambulizi ya kikatili ya vikosi vya Israel vinavyokalia kwa mabavu kambi ya wakimbizi ya Jabalia katika Ukanda wa Gaza.

Novemba 1, 2023 Jeshi la Israel lilidaiwa kuishambulia kambi hiyo kubwa na ya zamani ya wakimbizi ya Jabalia kwenye ukanda wa Gaza na kusababisha mamia ya vifo na majeruhi miongoni mwa idadi kubwa ya raia wasio na hatia katika ukanda huo.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Asia Baakodah ambaye ni Mkuu wa Idara ya Haki za Kibinadamu katika Ubalozi wa Kudumu wa Saudi Arabia ndani ya Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa huko Geneva nchini Uswisi.

Aliyasema hayo wakati akishiriki katika kikao cha taarifa cha Ujumbe wa Kudumu wa Waangalizi wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa huko Geneva kwa wataalam wa haki za binadamu.

Saudi Arabia ilisisitiza wito wa dharura wa kusitishwa kwa mapigano, kuachiliwa kwa mateka, kusitishwa kwa umwagaji damu, utoaji wa misaada ya kibinadamu, na kuzingatia makubaliano na sheria za kimataifa.(SG)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news