Serikali kujenga Kituo cha Forodha-Kakozi wilayani Momba

DODOMA-Serikali imesema inatarajia kujenga Kituo cha Forodha katika eneo la Kakozi lililopo Wilaya ya Momba mkoani Songwe ili kuunga mkono jitihada za kujenga Soko la Mazao la Kimataifa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Momba, Mhe. Condester Sichalwe, aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali wa kuweka Kituo cha Forodha, eneo la Kakozi Wilaya ya Momba, ili kuunga mkono jitihada za kujenga Soko la Mazao la Kimataifa.

Mhe. Chande alisema kuwa, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ina utaratibu wa kupitia na kufanya tathmini sehemu zote zinazoweza kujengwa Ofisi kwa ajili ya ukusanyaji kodi, utaratibu unazingatia uwiano wa gharama za ukusanyaji wa mapato na kiwango cha kodi kinachotarajiwa kukusanywa

"Serikali inaendelea kufanya tathmini ya kina katika maeneo mengi ikiwemo Kakozi, Wilayani Momba. Maeneo yatakayokidhi vigezo vya kujenga Ofisi za Forodha, taratibu za uanzishwaji wa Ofisi zitaanza kwa kuzingatia upatikanaji wa rasilimali watu na fedha,"amesema Mheshimiwa Chande.

Aidha, Mhe. Chande alisema kuwa tathmini hiyo itakamilika ndani ya mwaka wa fedha 2023-2024.

“Namuelekeza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aangalie uharaka wa ujenzi wa Kituo cha Forodha-Kakozi, Wilaya ya Momba endapo atajiridhisha kutokana na tathmini yake,"aliongeza Mhe. Chande.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news