DAR ES SALAAM-Serikali kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI) imefuta na kupunguza jumla ya tozo, ada na faini zisizopungua 232 kati ya 380 zilizobainishwa katika utekelezaji wake sawa na asilimia 61.




Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa Kikao Maalum cha Kikundi Kazi cha Mazingira ya Biashara Jijini Dar es Salaam, Dkt. Yonazi pia ni Mwenyekiti wa Kikosi kazi hicho. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dkt. Godwill Wanga na Kushoto ni Mwenyekiti Mwenza wa Kikundi Kazi hicho cha Mazingira ya Biashara, Bw. Vicent Minja.