Serikali yatoa shilingi bilioni 3.4 za maendeleo Mwanga

KILIMANJARO-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha shilingi bilioni 3.4 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara, elimu, miradi ya maendeleo, afya na vifaa tiba katika Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel alipomwakilishwa Waziri wa Fedha, Dkt.Mwigulu Nchemba katika kilele cha harambee na ibada ya kuadhimisha miaka saba ya Dayosisi ya KKKT Mwanga

Dkt. Mollel amesema kuwa, katika fedha hizo zilizotolewa halmashauri hiyo itanufaika kwa kupatiwa hospitali ya wilaya itakayosaidia kutoa huduma za afya kwa wakazi wa Mwanga na maeneo jirani.

Vile vile amesema kuwa, imesaidia kuongeza vifaa tiba, dawa pamoja na vitendanishi ili kuhakikisha wananchi wa halmashauri hiyo wanapata huduma za afya kwa usahihi na kwa wakati.

“Nitoe wito kwenu kuendelea kumuombe Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kutuongoza vyema na kutuletea maendeleo wana Mwanga na Taifa kwa ujumla,”amesisitiza Dkt.Mollel.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news