Serikali yatoa wito uraghibishaji wa huduma za chanjo

DAR ES SALAAM-Wizara ya Afya imekusudia kutoa chanjo kwa watoto zaidi 2000 ambao hawakupata chanjo na watoto 1700 ambao hawakumalizia chanjo huku wito ukitolewa kwa jamii kutoa ushirikiano watoto kupatiwa chanjo ili kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.
Akizindua rasmi Mfumo wa Uraghibishaji wa Huduma za Chanjo Wilaya ya Ilala, Dar es Jijini Salaam, Mkuu wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo, amesema watoto 2550 hawakupata chanjo kutokana na sababu mbalimbali na watoto 1753 pia hawakumalizia chanjo zao wilayani humo.

Amesema kwa kutumia afua ya uraghibishaji wa Chanjo kwa Viongozi wa Kijamii kupitia Programu ya "Human Centred design,HCD inayowezeshwa na UNICEF kwa kutasaidia makundi hayo mawili itakuwa rahisi kupata huduma kupitia mfumo huo kwa urahisi huku akiwapongeza Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, Ofisi ya Rais TAMISEMI, pamoja na Jiji la Dar Es Salaam kwa kuja na Programu hiyo.

Aidha, Mpogolo amesema ni muhimu kila mmoja kuweka mikakati kabambe katika kuhakikisha kila kila mtoto aliye na umri chini ya miaka 5 kupata chanjo katika kumkinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

“Kama unajua kuna maadui maradhi, sehemu kubwa ni kutengeneza mbinu, mimi niwapongeze sana Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma , pamoja na wengine kwa kuja na mfumo huu wa uraghibishaji sisi mmetupa daraja la kusimamia hivyo timu zote tusimamie vyema katika kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo katika kumkinga dhidi ya magonjwa”amesema.
Afisa Program ya Uratibu na Elimu ya Afya Maeneo ya Kazi kutoka Wizara ya Afya, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, Simon Zilimbili, amesema chanjo hiyo itaendeshwa kwa siku 10 katika tarafa mbili(Ukonga na Segerea) kati ya tatu za Wilaya ya Ilala ambapo kupitia mpango huo utasaidia kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo.

“Itakuwa ni rahisi kufuatilia kwa sababu kuna taarifa za kila eneo kuanzia ngazi ya mtaa hivyo nitoe wito kwa wananchi kutumia fursa hii kuwapeleka watoto kupata chanjo na zoezi hili litaendeshwa kwa siku 10,”amesema.

Kwa upande wake Mratibu wa Chanjo Halmashauri Jiji la Dar Es Salaam,Martine Kalongolela amesema lengo la zoezi hilo ni kufikia asilimia 100 huku akitoa hofu wananchi na zoezi na hali hiyo itasaidia kumkinga mtoto huku akitolea mfano madhara ya mtoto akikosa chanjo ya Polio ni kusababisha ulemavu au kifo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news