Social Action Trust Fund (SATF) yajivunia mafanikio makubwa miaka 25

DAR ES SALAAM-Taasisi ya Social Action Trust Fund (SATF) katika kipindi cha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake imefanikiwa kusaidia watoto 210,000 nchini kuwatoa katika mazingira hatarishi, kuwawezesha kujitegemea na kuchangia katika pato la taifa.

Shirika hilo lilianzishwa kwa udhamini wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Serikali ya Marekani April,1998 na kuratibiwa na Serikali ya Tanzania.

Akizungumza katika mjadala maalumu wa wadau wa taasisi hiyo kwaajili ya maadhimisho ya miaka 25, uliofanyika jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake wa mwaka, Ofisa Mtendaji wa SATF Beatrice Mgaya, amesema mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano mzuri kati ya taaisisi yake na wadau mbalimbali katika ngazi husika.

Amesema taasisi yake imekuwa ikifadhili elimu ya msingi, sekondari, ufundi na vyuo vikuu, huduma za afya, lishe, ulinzi wa mtoto, uimarishaji wa uchumi na kaya zenye watoto walio katika mazingira hatarishi, na kutoa msaada kwa Watoto wenye mahitaji maalumu.

Kwa mujibu wa Beatrice, msaada na ufadhili wa SATF umekuwa ukipitia katika sasasi na taasisi zisizo za kiserikali zinazoaminika ambazo zinatekeleza miradi ya SATF katika Halmashauri 36 za Tanzania Bara.

“Hii ni rekodi nzuri na ya kujivunjia na ninaamini kwamba SATF inatendelea kuisadia jamii kwa kuhakikisha watoto wetu ambao hawana uwezo wanafikia ndoto zao.

"Hadi sasa tuna wanafunzi ambao tuliwafadhili tangu ngazi ya msingi hadi chuo kikuu na wengine wameajiriwa, kwetu sisi hilo ni jambo la kujivunia,” amesema Beatrice.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya SATF Mariam Mwaffisi ameelezea kufurahishwa na hatua hiyo ya mafanikio huku akiumiminia sifa lukuki uongozi wa taasisi hiyo kwa utendaji uliotukuka.

“Mafanikio kama haya hayaji hivi hivi bali ni kutokana na uongozi bora na wachapakazi tulionao hapa SATF. Niwapongeze kwa hatua hiyo. Kama kuna mtu anataka kujifunza namna ya kuongoza aje SATF achukue mfano wake,”amesema Mwaffisi.
Mwenyekiti wa Bodi ya TASAF Bi. Mariam Mwafisi (kushoto) akishiriki katika utaoji vyeti kwa wadau mbalimbali. Kushoto kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa SATF Beatrice Mgaya na Meneja wa Miradi, Nelson Rutabanzibwa.

Katika maadhimisho hayo ya miaka 25 ya taasisi hiyo imetumia fursa hiyo kukutana na wadau wake kwa lengo la kutafakari mafanikio na changamoto ndani ya miaka 25 ya kuhudumia jamii ya Tanzania.

“Si hivyo tu bali tumeamua wakati wa maadhimisho iwe fursa pia ya kuendelea kuwajengea uwezo wadau wetu ili wapate ujuzi zaidi wa kuendelea kutekeleza miradi ya SATF kwa ufanisi bor zaidi,” amesema Meneja wa Miradi ya SATF, Nelson Rutabanzibwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news