TAA yakabidhiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)

KILIMANJARO-Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro umekabidhiwa rasmi kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) kutoka kwa iliyokuwa Kampuni ya Uendelezaji na Uendeshaji Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KADCO) baada mkataba wa uendeshaji kukamilika Novemba 9, mwaka huu.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya uwanja huo,Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa amesema, pamoja na mabadiliko hayo yaliyofanyika Serikali itazingatia stahiki zote za wafanyakazi zinalipwa kulingana na sheria.

“Kiwanja cha KIA ni kiwanja cha kimkakati pamoja hivyo pamoja mabadiliko yaliyofanyika tayari kuna kikosi kazi kinatakachohakikishwa viwango vya uendeshaji vinaendelea kukua na maslahi ya watumishi yanapatikana kulingana na Sheria za utumishi zilizopo,"amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa amesema kuwa, mabadiliko ya uendeshaji yaliyofanywa yanakwenda sanjari na maboresho katika usafiri wa anga yanayojikita katika ununuzi wa ndege mpya na ujenzi wa viwanja vya ndege ili kurahisisha shughuli za kibiashashara ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso amesema, ni wakati sasa wa Serikali kuhakikisha miradi ya ujenzi wa viwanja vya ndege ambayo iko chini ya Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) na TAA inasimamiwa kwa karibu ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na viwango.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara amewahakikishia wadau wote kuwa pamoja na mabadiliko hayo huduma zitaendelea kutolewa kwa kuzingatia miongozo na kanuni za kimataifa zinazooognoza usafiri wa anga.
KADCO ni kampuni iliyosajiliwa Machi 11,1998 kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni, Sura ya 212 ambapo Julai 6, 1998 Serikali iliamua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) uendeshwe kupitia sekta binafsi ambayo ilikuwa kwa njia ya ubia kati yake na Kampuni ya Mott MacDonald ya Uingerereza, South African Infrastructure Fund ya Afrika Kusini.

Sambamba na Kampuni ya InterConsult ya Tanzania) na mikataba miwili ambayo ni Mkataba wa Uendeshaji (Concession Agreement) pamoja na Mkataba wa Ukodishaji (Lease Agreement) baina yake na KADCO.
Mwaka 2010 kutokana na uendeshaji usioridhisha wa uwanja huo Serikali iliamua kununua hisa za wanahisa wenza wa KADCO kwa kuvunja Mkataba wa Wanahisa na hivyo KADCO kumilikiwa na Serikali asilimia 100 ambapo iliendelea kuendesha KIA ikiwa ni Kampuni ya Serikali kupitia Mikataba ya Uendeshaji (Concession Agreement) na Ukodishaji (Lease Agreement) ambayo ukomo wake ambao umefikia mwisho tarehe 9 Novemba, 2023 na 9 Novemba, 2023, Serikali imeamua kuhamisha shughuli za Uendeshaji kutoka KADCO kwenda TAA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news