Tanzania imepiga hatua katika masuala ya wanawake-Rais Dkt.Mwinyi

DAR ES SALAAM-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepitisha na kutekeleza mageuzi kadhaa ya kisera yakiwemo marekebisho ya hivi karibuni ya Sera ya Maendeleo ya Jinsia ya Tanzania.
Marekebisho ambayo yameweka mfumo wa kuimarisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake katika masuala ya elimu, afya, ajira na upatikanaji wa ardhi.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akifungua mkutano wa Mawaziri wa Afrika wanaohusika na fedha pamoja na jinsia kutoka nchi 22 wanachama kwa kushirikiana na Jukwaa la Usawa wa Kijinsia (UN WOMEN).
Sambamba na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF Afritac East) katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam leo Novemba 15,2023.

Mkutano huo utajadili kuhusu ufadhili wa usawa wa kijinsia. Nchi zinazoshiriki mkutano huo ni pamoja na wenyeji Tanzania, Burundi, Burkina Faso,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eritrea, Ethiopia, Guinea, Ivory Coast, Nigeria, Senegal, Kenya, Liberia, Madagascar, Malawi, Msumbiji, Somalia, Afrika Kusini, Rwanda, Sudan ya Kusini, Zambia, Zimbabwe na Uganda. Mashirika mbalimbali ya kimataifa wanashiriki mkutano huo unaoendelea hadi tarehe 17 Novemba.
Naye Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mwigulu Nchemba amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ni nguzo ya mafanikio kwa wanawake nchini kutokana na uongozi wake, pia Serikali imeendelea kupigania usawa wa kijinsia na kuwawezesha Wanawake nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news