TRA awards zafana

DAR ES SALAAM-Hizi hazikuwa Tuzo za Muziki, hazikuwa Tuzo za Filamu au Tuzo nyingine kubwa tulizozoea kushuhudia kila mwaka bali zilikuwa ni Tuzo za TRA 2023, Tuzo za Mamlaka ya Mapato Tanzania ambazo usiku wa kuamkia leo zimetolewa kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es salaam kwa kiwango cha kuvutia katika kuwatunuku Walipa kodi bora wa mwaka.
Ukiachia mbali rekodi mbalimbali ilizovunja Mamlaka hii chini ya uongozi wa Kamishna Mkuu Alphayo Kidata ikiwemo ya ukusanyaji wa kodi kwa kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa toka kuanzishwa kwake, Mamlaka hii pia siku hadi siku imeendelea kuweka nguvu kwenye kutoa elimu ya kodi na kutengeneza daraja zuri na rafiki kati yake na walipa kodi kote nchini na sasa imekuja na ubunifu wa kipekee wa kuwatunuku waliofanya vizuri kwenye kulipa kodi kwa hiari.

Washindi wa kitaifa kwa ujumla waliopongezwa kwa bidii zao za kulipa kodi kwa hiari katika Tuzo hizi za TAXPAYER APPRECIATION AWARDS 2023 ambazo Mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko, ni Benki ya NMB iliyotajwa kama Mshindi wa kwanza huku Mshindi wa pili akiwa ni Tanzania Breweries Limited (TBL) na wa tatu akiwa ni Benki ya CRDB wakati Benki ya NMB ikitajwa tena kuwa Mshindi wa jumla.

Kwenye hotuba yake fupi, Kamishna Kidata alisema baadhi ya vigezo vilivyotumika kupata Washindi ni rekodi nzuri ya utunzaji kumbukumbu za kodi, uwasilishaji ritani sahihi kwa wakati, kulipa kodi sahihi kwa wakati, ulipaji wa kiasi kikubwa cha kodi na kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania pindi inapohitajika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news