Tume yajipanga kupaisha uchumi wa nchi kidigitali

LINDI-Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama, Mkundwe Mwasaga, amesema wamejipanga ili kuhakikisha uchumi wa Tanzania unakua zaidi kupitia uchumi wa kidijitali.
Katika wasilisho lake kwenye Mkutano Mkuu wa Saba wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania-TEF, unaofanyika Mkoani Lindi, Mkurugenzi huyo Mkuu wa Tume ya Tehama, amesema tume hiyo itahakikisha inakuza tehama hapa nchini.

"Sekta ya tehama ni muhimu nchini na ni mtambuka hivyo juhudi za pamoja zinahitajika sana hapa nchini.

"Tutasajili na kukuza wataalamu wa tehama nchini na kuwapeleka nje ya nchi ili kupata fursa zaidi,"amesema Mwasaga.

Aidha amesisitiza kuwa watawajengea pia ubunifu wataalamu kwa kuanzisha au kujenga vituo vya ubunifu katika Mikoa minane nchini Tanzania.

Kwa kuanzia amesema wataanza na mikoa minane ikiwemo ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Lindi, Tanga, Mwanza, Mbeya na Zanzibar. Mipango iliyopo ni kuhakikisha vituo vya aina hiyo vinajengwa katika kila wilaya nchini ili kuwafikia zaidi Watanzania katika kila pembe ya nchi.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama (ICTC), Dk. Nkundwe Moses Mwasaga, akiwasilisha mada kuhusu TEHAMA katika Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Uwanja wa Ilulu, Lindi uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Novemba 13, mwaka huu.

Amesema kila kituo kitahudumia kampuni zaidi ya 200 lengo ni kuhakikisha Tanzania inashindana kwenye uchimi wa kidijitali.

"Jamani pia tunafanya utafiti ili kujua kama sera za masuala ya Tehama zinafanya kazi ipasanyo na ikiwezekana zikafanyiwa mabadiliko makubwa".

"Akili bandia imekuwa ni changamoto duniani, hivyo tume ya tehama inaifanyia kazi kwa haraka. Tutahakikisha mifumo yote inasomana nchini na kila mtanzania kuwa na namba moja," alisema Mwasaga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news