ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi, ameshukuru ushirikiano wa karibu uliopo baina ya Tanzania hususani Zanzibar, na Benki ya Dunia (WB),Umoja wa Ulaya (EU) na ushirikiano wa diplomasia uliopo baina ya Australia na Tanzania.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alitoa shukurani hizo Ikulu jijini Zanzibar alipozungumza na wageni hao walioambatana na ujumbe waliofuatana nao kwa nyakati tofauti.
Alisema, taasisi hizo zina mchango mkubwa wa maendeleo ya Zanzibar hasa kukuza sekta ya Afya nchini, Elimu, Utalii na Uchumi wa Buluu.

Pia, Rais Dk. Mwinyi alimueleza balozi huyo azma ya kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Austalia na Zanzibar hasa kwenye masuala ya uwekezaji, biashara na utalii.

Alimueleza Mkurugenzi huyo, Uchumii wa Buluu ni sekta muhimu kwa uchumi wa Zanzibar na kuongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inafanya kila iwezavyo kunufaika na fursa zinazotokana na sekta hiyo kwa ajili ya uchumi na watu wake.
Aidha, alimueleza mgeni huyo kuimarisha zaidi ushirikiano wao kwenye sekta hiyo, ili kujenga uweledi kwani idadi kubwa ya Wazanzibari wamejikita zaidi na masuala ya uvuvi na ajira zinazotona na bahari.

Kwa upande wao wageni hao walemueleza Rais Dkt.Mwinyi juu ya kuendelea kuiungamkono Zanzibar na Tanzania kwa ujumla hasa kwenye masuala ya kuendeleza ushirikiano wao wa diplomasia na kuona fusra za uwekezaji na uchumi zilizomo Tanzanzia vinanufaisha pande zote na ushirikiano wao.